How I Built My Juice Biz
Can You Start a Juice Biz with Less Capital?
“Start capital ilikuwa Kes 5,500, 3,500 ya kutengeneza stand na ku-source juice… so tulianza tu basically na mitungi mbili: Passion na Mango juice.”
"Mtungi moja ilikuwa 4,500… transport ya kwenda town kurudi so inakuja roughly 5,500.”
Where Did the Juice Biz Idea Come From?
“So, idea ili-start from, ilikuwa tu mental. Ilikuwa tu unashinda kwa nyumba ku-trade pale forex. Nikitembea, siku moja nikitafuta juo sana.. eh nikakosa. So nikaangalia hiyo ni job opportunity.”
How Do You Get Your First Customers in a Juice Biz?
“The first client in fact nilipata saa nane halafu alikuwa client wa juo ya chwani. The first day niliuza 150 shillings manze. Hizo zilikuwa tumblers tatu. The first client nilipata saa nane, wa pili nilipata saa kumi, na wa mwisho hadi ni msee alinipitia akanipata nikifunga. Ati alikuwa anadai nimpee juo za display for free, but manze ikabidi tu nimemshow ni biz ndio naanza akanielewa akani-support zaidi.”
What Happens When You Feel Like Giving Up Early?
“Eh.. the second day manze sikufungua nilikuwa nime give up. Nilikuwa nimechoka akili. Najiangalia najiuliza.. do I really need to do this manze? Because nikiangilia sales za first day, 150 shillings it was so disappointing manze..”
“Nikarudi nikafikira tena, nikaona this is an opportunity ya ku-strategize about this thing... because you don’t give up when it’s the start.”
How Much Can a Juice Biz Make Per Day in Kenya?
“Siku zikiwa down unaeza make sales za at least 3,500 hapo in a day.”
“Unaeza piga hadi sales za 7k.”
“So total averagely in a week unaeza kuwa una make 50k.”
What Money Habits Help You Grow a Small Biz?
“Savings saves a lot… jaribu ku-save kama ni 10bob unapata. Ile time una ignore pesa kidogo kidogo hizo ndio zinakujaga kukuwa big within a period.”
What Are the Toughest Challenges in a Juice Biz?
“The toughest thing ku-run biz ni pale kwa mahesabu… ukipiga mahesabu zineza kupiga chenga. Huna ile accurate value… hii ndio profit, hii ndio nitalipa wasee, hii ndio nitafanya investment.”
“But you learn with time. Unajifunza na ma-mentors, wanakusaidia ku-grow yani.”
What Are the Low Seasons for a Juice Biz?
“Low season inakuwanga ile time ya mvua manze… juu basically tunauza juice baridi.”
“Una use that opportunity ku-market WhatsApp to other clients. Unaeza source other clients from online from social media platforms zozote tu uki-market biz. Unapata clients despite the situation vile iko.”
What Mistakes Should You Avoid in a Juice Biz?
“The biggest mistake nishaifanya ilikuwa impulsive buying. Nilienda nika source a juicer. We really needed a juicer, lakini sikujua how it works. Nikakuja the first tumenajaribu ku-try ku-work nayo, it was very difficult manze.”
“I learned from it. Before you get to buy something in biz, get your time to know. Do you really need this thin? Halafu pale ukishachukua mzigo unafaa ukuwe unajua kama unaeza itumia juu unaeza buy kitu ukakuja kukaa nayo bila kuitumia and that’s money gone. Money gone cannot be recovered.”
What Advice Would You Give Someone Starting a Small Biz?
“Msee anaezadai ku-start a biz, start with what you have.”
“Hakuna time itawahi fika ukuwe na that big you need to start.”