logo

How To Sell On E-commerce Sites Like JUMIA

 Text graphic of selling strategies for online marketplaces.

JUMIA ni one of the big e-commerce sites in Kenya na hata Africa. Ina-bring together millions of buyers as customers na sellers wenye biz zinauza bidhaa different.

Iko na three main parts ambazo ni the marketplace where wasee husell and buy, JUMIA Logistics for deliveries, na JUMIAPay ya kuwezesha payments.

Advantage ya kuuza on JUMIA, ni that unaweza fikia more customers beyond mtaa yako. Pia, huhitaji kujishughulisha na delivery ya products zako because Jumia takes care of that.

Pia wanapea customers wako an easy way to pay for products zako through JUMIA, which means that watakuwa na an easy time na watakutrust more, na hii inaweza increase sales zako.

JUMIA ina believe that wanamake maisha ya wasee easier by kuallow online shopping na pia wanacreate more opportunities for businesses kujikuza na for mayuts kujitengenezea jobs na hustles in e-commerce.

Getting Started

 Image displaying Jumia sign-up page.

Step 1: Register 📖

Kuget started register on the JUMIA Vendor Platform.

Utajaza registration form na kusubmit the required documents: hizi ni Business Registration certificate na your Bank Account Details.

Step 2: Practice kuwa an e-commerce expert 🧑🏽‍🎓

Kuna training ya sellers wapya offered by JUMIA unahitaji kucomplete kisha you activate your Seller Center Account to manage your shop.

Step 3: Kuweka na kuuza products zako 🥳

Upload your best selling products alafu anza kuuza.

Step 4: Access free promotions na marketing by JUMIA 🤑

Hapa unaweza pata more views kwa store na products zako kutoka campaigns na promotions za JUMIA.

What Do You Need To Know?

Commission.

JUMIA hulipisha sellers wao commission between 6% and 20% depending on category ya products ambazo unasell.

Unaweza angalia exact commissions for different products hapa:https://vendorhub.jumia.co....

Shipping Cost Contribution

Hii ni cost ya lazima for sellers kuchangia for deliveries kwa customers.

For example, hapa Kenya hii fee ni between KES 25 for small parcels and KES 300 for very large parcels.

Cheki the exact shipping cost contribution fee hapa:https://vendorhub.jumia.co....

Ensure Price Yako Ni Competitive

Kumbuka that unahitaji kuadd the 6-20% commission as well as ile shipping contribution fee ya KES 25 -KES 300 to the final price of your items pale JUMIA.

Alafu cheki, bei yako bado ni competitive? Kama uko competitive, poa. Chapa biz 👍🏽👍🏽

If not, hautamake sales design unaexpect. Badilisha bei yako ama cheki kama unaweza pata products zako na bei afadhali kutoka kwa supplier.

Jaribu kuuza products ambazo uko na competitive prices ama vitu unique customers hawapati kwa watu wengine.

Hakikisha Uko Karibu Na One of JUMIA's Parcel Drop-off Locations.

Hii inamaanisha that unafaa kuwa karibu na city kama Nairobi ama town kubwa ambayo iko na parcel drop off ya JUMIA.

Kucheki hizi locations ziko wapi, search kwa “JUMIA Vendorhub” ya your country, for “vendor drop off locations” — kuna 7 in Nairobi.

Jua Kutumia The JUMIA Seller Centre

Management yote ya online store yako utaifanya kupitia the Seller Centre. Hii itakuallow kuona na kuaccess sales zako, kuongeza products unauza, na information ya hizo products.

Kuwa Patient

After kupost your first product itachukua kama one week ili rep wa JUMIA areview store yako na kuiapprove. After that uko live na unaweza anza kumake sales.

Ngoja Welcome Email Kutoka JUMIA.

Hii ni email itakuja kushow uko approved na unaweza anza kuuza on JUMIA na any other instructions ama tips unaweza hitaji.

Kuwa Aware of Stick Yako Na Inventory.

Kama unauza the same products kwa shop yako mtaani as on JUMIA, hakikisha unaupdate stock levels zako on JUMIA regularly usijipate kwa blunder ya kuwa out of stock.

Seller Score

Ukiuza on JUMIA, utakuwa rated between 1 and 5. Hii ni ya kushow performace yako kama seller.

Hakikisha unakeep stock levels up to date, na unadeliver goods zako on time ili kupewa a perfect score. Score mbaya itapunguza customers wanaona products zako.

Sales Performance

Kwa Seller Center, utaona section ya ‘reports’. Hizi zitakushow zile products zinaonwa mara mob na zile zinanunuliwa most. Hii inaweza kusaidia kuchagua nini utaendelea kuuza na ni nini utatoa.

“This training course was designed and supported by Strive Community, a global philanthropic initiative developed by Mastercard Center for Inclusive Growth and Caribou Digital.”

Umekuwa ukidream of starting your own online shop in kenya. Labda unauza parts na accessories za magari, beauty products ama nguo. Before uanze, utabenefit kujua itakucost doh ngapi.

Umekuwa ukidream of starting your own online shop in kenya?