Is Being a Barber a Good Biz?
Why Did Eric Choose Barbering as a Biz?
“Kitambo kidogo, miaka ya zamani, mimi nilikuwaga na ile hamu ya kufanya hii job, juu ndio job inatambulikana sana kwa mavijana nayo kinyozi ilikuwanga inapata ma customers wengi. Nilikuwa naona hapa naeza pata opportunity kubwa.”
“Ilikuwaga job ya msee nilikuwa namfanyia job, ki bahati, akasema joh anahama anaenda place ingine so mi nikachukua ile opportunity ya hapa ndio naeza wezea.”
How Much Capital Do You Need to Start a Kinyozi?
“Capital ilikuwaga ya 70k, na juu mi ni youthman, alinielewa akanifanyia na 65k, so I had little amount yenye nilikuwaga nayo kwa mfuko na through friends na parents kidogo wakani support, juu nilienda kwao nikajibonga na wakanielewa. Wakasema kama hapo ndio umeamua hapo ndio focus yako iko, haina shida tutaku-allow na tutaku-support.”
How Do You Attract and Retain Customers in a Kinyozi Biz?
“So, costumer wa kwanza ni wewe u-maintain, mi nilikujaga nikapata customer wa kwanza, nikampatia service poa. The more you do the service in a good way kesho yake anarudi, na anakuja na marafiki.”
“So, customer akipita anaona kuna kinyozi.. nini nini... the more it grows na the more inaendela kukua.”
Why Is Saving Important in This Kind of Business?
“Doh yenye tunapata hapa hivi we save, juu hatujui kesho venye itakuwa, so the little that we are getting, shughuli ni mingi za kufanyia hio doh. So, we save because we only know kuna days zinakuwaga na emergency.”
What Challenges Do Barbers Face?
“Kwa hii biz yenye sisi hufanya, competition ni mingi… saa zingine inabidi ume lower the standards kwa wale wenye hawawezi fika ile bei yenye huwa nataka.”
“Shida zenye tunapitia kama watu wa kinyozi, kwanza time ya arrears na restoking za vitu, kuzipata ni ngumu sana…ndio maana tuko na record, unajua by the end of that month doh imeenda wapi…”
“Low season zangu zinakuwaga during weekdays, achana na weekends. Weekdays tunajuanga mchana mnaeza stay hivyo, bila ma customer, lakini during the night unaeza pata mmoja-wawili-watatu-wanne hivi. At least ukisema hivo na uweke na doh yenye sisi tunalipisha at least unajipata uko pahali.”
“Ile machine yenye wewe unatumia personal, you have to take care of it vibaya sana…Ukikosa kui-take care iharibike kidogo itakugharimu doh mingi, of which hii machine moja kutengeneza ni almost 3k plus.”
How Much Can You Earn from a Kinyozi Business Weekly?
“Kwa ile wiki yenye umeamka poa God-willing unaeza pata 3500 kwa wiki… wiki ikiwa mbaya waeza jipata umetoka na kapa mbili ama umetoka na 1500.”
What Advice Does Eric Give to Aspiring Barbers?
“Kwa msee mwenye anataka kuanza hii biz lazima ukuwe na passion na kitu unapenda ama ni kitu unataka kuifanya. Sio useme tu unataka kuifanya juu watu wanafanya, hapana…”
“...lazma ujue how to treat your customers juu hapa tuna deal na ma-clients una make sure the next time akirudi anarudi akijuaga nakuaga na base yangu yenye siezi kosa kwenda kunyolewa.”