2018 NILICHIMBA MITARO ZA FIBRE OPTIC 🤗
Nimekaa hivi nikakumbuka 2018 pale Nyabs, I mean St. Philips Nyabondo 😅.
Nikiwa Form 4, nilikuwa nimefukuziwa school fees. Sasa opportunity ikajitokeza nikaconnectiwa job ya kuchimba zile mitaro za kuweka fibre optic cables za Safaricom pale Oyugis, Njianya kuelekea Karabok Secondary na hizo maeneo.
Nikajisemea, kwani ni kuchimba tu?
Wueh! Nilifanya hiyo kazi for like a week... na hiyo one week ilinifunza enough.
Jua liko juu ☀️, Saruru, spade na jembe mkononi, udongo mgumu, mwili imechoka, alafu kesho unaamka unajua bado kuna mtaro ingine inakungojea.
Kuna time unafika mahali unaangalia tu hiyo mtaro mbele yako unajiuliza,
"Hii fibre optic watu watatumia internet siku moja, lakini watajua kweli tulichomoa hii cable ground?"
Na hapo ndio nilijua kuchimba mtaro si mchezo. Definitely haikuwa ya kila mtu.
But looking back, kuna kitu napenda kuhusu hiyo experience. Life haikuonyesha mapema vile journey yangu itakuwa.
Nilikuwa Form 4, school fees imenifukuza shule, na niko Oyugis nachimba mitaro za fibre optic.
Fast forward to today, niko kwa IT, software engineering, AI na technology. 💻
Funny enough, ile fibre optic nilikuwa nachimbia ndio infrastructure ya watu kuconnect internet. Leo mimi niko upande ingine, najenga na kusupport systems zinazotumia hiyo connectivity. 🌐
Life huconnect dots aje sasa?
Sometimes unaishi moment bila kujua itakua part ya story yako years later.
Na respect kubwa sana kwa watu wa ground wanafanya hizi jobs kila siku. 👊🏾
Mimi nilikaa one week tu nikasema, "Wacha hii industry iendelee bila mimi." 😂
2018 ilikuwa character development proper.
From digging trenches for fibre to building technology. Kumbe dots zilikuwa zinaanza kuconnect mapema. 🔌💻
#TekliniTechnologies