2022 nilianza biz ya mitumba Gikomba. Nlitafuta 15k, nikachukua bale moja ya jeans na manguo zingine kadhaa .
Wiki ya kwanza ilikua moto coz nilikuwa nasort kwa nyumba, napiga picha na simu ya Tecno, nikiweka status. Sales zilikuwa somehow poa so nilifikiria nimefika.
Then shida ikaanza. Nilikua na post tu online, sikuwa na shop. Customers walikua wanabuy alafu wanahepa. Another thing kwa stock sikuwa najua grade A na grade B. Bale ilikua imejaa manguo na jeans zimechapa. Profit ikaanza kuwa losses. Kitu ingine sikuwa nayo ni patience.Nilikuwa nataka pesa haraka but after 2 months biz ikaenda mbaya, pesa ikaisha, motivation ikaisha pia.
Nimekam kurealize hustle ya mitumba inahitaji capital ya shop, kujua supplier poa, na uvumilivu. Location na customer trust ndi kila kitu.
Sijarudi bado kwa mitumba, but nimechukua hizo lessons kwa hustle.