
AISEE UNAVOPANGA KULIPA KISASI CHIMBA MAKABURI MAWILI-MOJA LAKO
-
Mwenye saa moja ukimuuliza muda atakutajia sawa sawa - mwenye saa mbili ukimuuliza muda hatokuwa na hakika.
-
Usikae chini ukaangalia ulipo shindwa - angalia ulipo teleza.
-
Hakuna mahali utakapo pata Amani kama si kwako mwenyewe- hata kwa sangoma hakuna.
-
Binadamu wata kuwekea mashaka kwa yale unayosema - wataamini utakayo fanya tu.
-
Kuwa mwema kwa walio chini wakati unaelekea juu - utawahitaji siku utakapo shuka chini.
-
Muda ulio furahia kuupoteza -haukupotea ( muda haupotei)
8.usijielezee sana kwa marafiki hawaitaji maelezo yako - maadui hawatokuamini pia. (Fanya unavyo weza)
-
Ujasiri sio kukosa woga - uwezo kutenda unapokutana na woga.
-
Jitahidi kukua bila kujali kupita urefu wa baba yako ni kiasi gani.
-
Njia nzuri ya kutabiri mambo yako yajayo ni kujenga sasa hivi.
-
Ni bora kuchukiwa kwa jambo ulilo nalo kuliko kupendwa kwa jambo usilo nalo.
-
Usijali juu ya uliokuwa nao kipindi cha nyuma , ni sababu pekee ya kwa nini haupo nao sasa hivi- usijute
-
Furaha ni faida kuliko utajiri- hakuna anayeweza kukuazima.
-
Kila jambo hutokea kwa sababu
-
Msamaha sio kitu unafanya kwa ajili ya uliye mkosea- unasamehe ili uwe huru na uweze kusonga mbele wewe binafsi.
-
Tofauti unayo iona baina yako na mwingine ndio uzuri wako
@nabiimswahili