
Chenye najua ni ati wasee mob wakianza kutengeneza content, wao hutumia sana sana app ya Kinemaster kuedit videos zao. Ubaya ni inatokanga na watermark yake kwa videos zako bana. Alafu sasa wakianza ku advance wanaingia Capcut. Hii nayo imerahisisha mambo ju nliona unachagua tu templates alafu inakufanyia editing videos zinatoka kali kali ๐๐ฏ. Tiktok nayo sikuhizi nmeona wame'incooperate Capcut so ata kaa we ni amateur kazi yako inatoka edited clean. But sasa unaona huezi rely on hizi templates ju saa zingine hazitatoa video venye unadai. Inabidi umejifunza tu.
Lakini kuna some very cool apps unaeza ivishia kuedit watu wakutii akiyanani. Wachana na Kinemaster na Capcut, umeskia App inaitwa Alight Motion? Noma sana๐ฅ. Wacha hio ata, my favourite hukua VN Editor. Hii inakuanga na editing tools zingine kali sana. Editing timeline hukua user friendly na pia colour grading nayo pia si mchezo. Chenye hua kinani'nice ni hapo kwa kuedit speed za clips, unaeza customize some parts za scenes ziende in slow motion alafu ivuke iende na 2x speed. Sijui kaa mnanirada but unaeza edit scenes kama za Rambo buana. Ama nyi wasee hua mnatumia mobile apps gani ku edit videos?
