El Nino Hustle Chances
Mvua kubwa huleta shida, lakini pia huleta demand mpya. Watu wanahitaji: gumboots, umbrellas, raincoats, heavy jackets, duvets, carpets, doormats, warm socks, hot drinks, uji power, tea masala, thermos flasks, charcoal, gas and firewood. Hii ni time ya kuuza “protection and warmth,” si fashion peke yake. Kabla mvua ianze vibaya, unaweza stock kidogo hizi items or hata chukua orders in advance kwa estate, workplace, church na online.
El Nino pia inamaanisha barabara mbaya, foleni na watu kutotaka kutoka nje. Hapo delivery services zinashine: food delivery, groceries, gas, water, medicine, school supplies. Cleaning and drying services za carpets, sofas, shoes and clothes zinaongezeka juu ya matope na damp. Think also housing side: simple repairs, fixing leaks, drainage unclogging, sandbags, plastic sheeting. Swali kwa Meshers si “mvua itadumu hadi lini,” ni “watu wakianza kulalamika juu ya mvua, mimi naweza kuwauzia suluhisho gani?”