
Hadith Fupi Iliyonipevusha.⭐
Hadija mwenye umri wa miaka 24, baada ya kumaliza chuo kikuu Cha ufundi, anaamka asubuhi kufanya shughuli zake za Kila siku nyumbani. Kufagia, kupika, kuosha vyombo, kupiga deki nakadhalika.
Siku moja alimuuliza nyanya, Nyanya Mimi naweza kufanya kazi serikalini? Nyanya akamtazama na kutabasamu. Akamjibu' unaweza kufanya, lakini wewe unaonekana mwanabiashara mkubwa sana. Bibi akatoa shilingi 500 za Kenya alizo zihifadhi kwa miaka miwili, akampa na kumwambia ' nenda ukanunue mboga za kienyeji ukalete hapa'. Alipoleta waliketi chini pamoja na kuanza kufunga vidude vidogo vidogo. Haya basi. Tembeaa kijijini ukiuza. Hadija alikuwa muoga lakini alitii amri ya nyanya.
Kwa kuwa kijijini walimjua nyanya, walipomuona mjukuu wake akiuza mboga walinunua bila wasiwasi. Alirudi nyumbani na shillingi 900 za Kenya. (Kisa kitaendelea)
Mafunzo. *Akiba haiozi. *Mwanzo mdogo lakini piga hatua. *Jiamini *Hatua mia moja huanza na hatua moja.