
It had been one month of house hunting and all houses looked expensive. Hio siku nimezunguka the whole day vumbi na njaa imenitwanga ajab ikabidi niingie kibandaski hapo nikateremsha Ugali mayai before minyoo ianze kuitana mkutano ikidhani host alienda kwa baba. Nikitoka tu hivi nikaona a poster hapo inasema vacant houses available. Mimi ju nlikua nataka bedsitter nikachukua number faster nikacall. Nikamuuliza naeza pata bedsitter? Akasema Yes ziko, acha nikutumie picha. Teke akasukuma pic WhatsApp nikaona ni a good one, Rent? Akanishow 6k. Haa nimeangukia bana naeza pumzika. Nikaulizia the process ananishow lazima deposit na rent I pay, but because kuna madam mwingine anapigania hio keja anataka kuingia chenye ntafanya, ni nitume deposit mapema nibook ndio niwahi. Akanitumia hadi directions nikifika hapo nje I call atokee. Buana nayo kwa ngeli hakubahatisha, Alinipiga kiswahili nikamtumia a staggering 60 dollars. Sasa kufika penye alinidirect buana hakuna ata flats. Kwanza ata nlipata woria fulani walikua wanauza mali mali hapo and some second-hand items. Na mkamba fulani hapo anauza mtura. I call the number naskia its not in service. I call again, and again then sasa the shock and realization hit me, its a scam. Nikauliza huyo msee wa mtura kama kuna rentals around zenye ziko vacant. "mbloo unataka zile za mambati sambambu ndio ziko tu" Nikasema hapana thanks. Nlijam vibaya sana nikakula mtura ya 200. Huyo mkamba alicheka sana nikimpigia hio story. Akanishow nimekaribishwa Nairobi. What I learnt ni ukiona hizo posters za vacant houses usikubali kuwapea pesa before uone keja and some documentation.