Jana tukiwatch game ya Japan na Netherlands niliona kitu ilinifascinate sana. Kulikuwa na youth mmoja anauza wristbands za rangi tofauti za countries mbalimbali. Alikuwa ame-embed majina kwenye hizo bands na kusema ukweli, huyo comrade alikuwa professional! Kwa beadwork nampea 10/10. Alikuwa na accessories nyingi na cha kushangaza ni kwamba nyingi alikuwa anatengeneza hapo hapo ukiwa unaona process yote. Nikamuuliza alijifunzia wapi hii skill, na jibu yake ilinichekesha kidogo. Alisema alijifunza tu baada ya kuona wengine wakifanya. Hii ni side hustle kwake, lakini inaonekana inalipa. Swali langu ni: Kuna mahali mtu anaweza kujifunza hii art professionally? Na je, inaweza kuwa biashara nzuri ukilenga tourists na foreigners wanaotembelea places kama Giraffe Centre na Nairobi National Park?