
Kuna boyz wangu alikua anarauka ngware nikimuuliza anaenda wapi anasema ni mission tu anaenda. Msee alikua analia mashida buana hakua na 5 bob kwa mfuko. Ata nlikua nashindwa anasurvive aje na anakaa mtu ako na job ju alikua anadunga official. Kufanya investigation kumbe anafanyia job photographer na videographer mwingine hapo. Kazi ilikua kukua mtu wa mkono na kurun errands hapa na pale. Nlishangaa akiniambia ati ye hua halipwi ni experience anasaka tu aanze photography firm yake. Nikasema ní urímú. Lakini kumbe alikua amekachora. Alitoka hapo na experience na connections kibao. Sikuhizi namwonanga akiwa anapost huko WhatsApp kazi yake safi safi na saa zingine roadtrips za Naivasha. Yeye alishaakafunga buana. Juzi aliniambia pia mimi naeza anza kuvolunteer in my field nisake connections. Lakini nayo nisilete kiburi buana wanaeza niharibia all my connections. Mantain tu hapo na nikue humble. We unaona aje hii story?
