Leo nimeamua kuongelea hii coming Finance Bill ju mambo si mazuri hata kidogo 😕. Saa hii round imefika kwa wasee wa mtumba biz na viatu. Serikali inapanga kuongeza taxes kwa bidhaa zinazoingia nchini na mwisho wa siku ni hustler wa kawaida ndiye anabeba mzigo.
Mtumba ndio imekuwa source ya income kwa maelfu ya youth Kenya. Watu wanauza viatu, nguo, bags na wanajikimu kupitia hiyo biashara. Lakini taxes zikiongezwa, bei ya mzigo itaenda juu, customers watapungua na biashara nyingi zitakuwa ngumu kusurvive 😔
Imagine ku-import bale ama stock ya viatu halafu ushuru iko juu, transport juu, rent juu na bado customer anataka bei poa. Hustler anabaki katikati akiwa confused vile atasurvive.
Na hii ndio biashara imekuwa ikisaidia vijana wengi kujiajiri instead ya kukaa jobless. Serikali inafaa kufikiria youth na small businesses before kuongeza taxes kila mwaka. Si kila solution ni kuongeza ushuru kwa mwananchi wa kawaida.
Meshers wenye wako kwa mtumba biz na viatu, mnaonaje hii coming Finance Bill? Itaaffect biashara yenu aje? #Kujengana