Meshers, nimeona vile Wakenya wanacheka na kufanya jokes kuhusu baadhi ya hustles za Wakenya wenzao. 😂💔
Comrades, kama unapiga hustle yako kihalali, unatafuta pesa ya kujikimu na kusaidia familia yako, kwani kuna haja ya kuskia aibu? Whether ni kuuza mayai, kuosha magari, kubeba mizigo, kuuza smokies ama kufanya kazi yoyote halali, hakuna hustle ndogo ikiwa inakuingizia pesa safi. 💯
Tusikue watu wa kudiscourage wengine juu ya vile wanatafuta pesa. Leo unacheka hustle ya mwenzako, kesho unaweza kujipata kwa situation yake.
Aibu si kufanya hustle. Aibu ni kudharau mtu anayejituma kutafuta riziki. 🔥
Meshers, tusichekeane, tujengane! 🤝❤️
#kujengana #HustleWithDignity
0
0
0