Nimeona youth flani akilalamika ameenda almost 5 hours bila kupata sale hata moja 😒. Nimefeel pain yake. Alikopa KSh 500 kwa friends na family, akanunua products za kuuza online. Kwa hizo 5 hours zote amekuwa online akipost, akimarket na kujituma, lakini hakuna order hata moja. Ni mtu mmoja tu aliuliza bei, akanyamaza na hakurudi tena. Hii biashara si mchezo bana. Watu huona sales na profits lakini hawajui zile masaa unaeza kaa bila customer hata mmoja. Kwa wale mko biashara, longest mliwahi kwenda bila kupata customer ilikuwa masaa mangapi ama siku ngapi? Na mlijipea moyo aje msikate tamaa? 🤔
0
0
0