
Permit / License Kuna Mesher aliuliza swali fiti sana hapa mesh. What's the difference between the two? Not like niko na ultimate correct answer, but niko na views kiasi nime research hapa na pale. Halafu zile common Licenses na Permit za ku run biz hapa nchini ni gani na gani? Will list a few zenye najua so please add more tujengane kama wanajamii.
Mwanzo kabisa, License ni kibali chenye upeanwa kwa biz, individual, institution, organisation ama firm ya ku'iruhusu kufanya activity ama biashara flani. Na hii inaeza toka kwa wizara, county ama national gova. Nayo Permit ni ile idhini individuals upewa kuonesha ame qualify kufanya kazi, biashara ama ku qualifify kuendesha activity flani na hii ukuwa very restrictive in nature. Kwa mfano msee wa chemistry, daktari, mjenzi na kadhalika. So permit iko restrictive, needs certain qualifications, inaeza kuwa easily withdrawn & prone to lots of inspection, nayo license iko more open to anyone mwenye anadai. Hii nikutokana na uelewa wangu. I might be wrong through.
Nchini tuko na zile common License nazo nikama:
Single Business Permit
Alcohol and Liquor License
Fire and Safety License
Driving license
#Film classification license
Music Copyright License
Communication Authority License
Na most of hizi ukuwa renewed annual.
Then common Permit ni kama;
Health Permit
KRA permit
Nema Permit
Kama unamaoni please share kwa comment ndio tujifunze sote.
