
Sample of my shairi
NIMEMPATA Kwa kushuka na kupanda, milima kuparamia, Nikisaka 'nayependa, malengo ya familia, Matatizo njia panda, kuvuka mito 'kalia, Kichwani mwangu jazanda, picha 'nayotarajia,
Mungu baba wa matendo, akanifikisha kwake, Mtoto mwenye upendo, na heshima kwa wenzake, Kwa mapenzi ana nyendo, na tabia wema wake, Mwenye hutu si magendo, mbona nisiwewezeke,
0
0
0