Shiquo amekuwa akiuliza mbona siku hizi videos zake zinafika 100 views na likes mbili, ilhali kitambo alikuwa anavuta hadi 300K views.
Naona shida inaweza kuwa hii...
Wengi wetu hatukumfuata juu alikuwa anauza luxury items. Tulimfuata juu alikuwa anatuletea deals za "hii nayo hata Fuliza inaweza."
Leo ukiingia live unakuta bidhaa nyingi ni zile zile unaona Garden City, Two Rivers ama supermarket... tofauti ni bei imepanda sana.
Walahoi tulikuwa tunangoja zile offers za:
Perfume za "bei ya lunch." Viatu za "salary haijaingia bado." Sufuria za "ukijikaza kidogo unaenda nazo."
Labda ndio maana engagement imepungua. Audience iliyompea spotlight ilikuwa inatafuta affordability, si premium products.
Ama mnaonaje Meshers? Je, creators wakibadilisha target market huwa wana-risk kupoteza audience yao ya kwanza?