@Team mesh Acha niache hii apa inaweza saidia mmoja ama watu kumi🙏❤️ JINSI YA KUANDAA KAHAWA CHUNGU(thungu) ❤️
Tuseme tunapika ya watu wawili
Viungo
• Maji vikombe 4
• Kahawa vijiko 2
• Tangawizi kijiko 1
• Poda ya Cinnamon kijiko 1/4
• Iliki iliyosagwa kijiko 1/4
• Karafuu nzima vipande 2
• Kongomanga kiasi
Maandalizi
• Changanya viungo vyote kwenye sufuria na uongeze maji.
• Bandika kwenye jiko la moto na upike kwa dakika 13 au 20.
• Punguza moto na upike kwa takriban dakika 3 kisha uepue na kutia ndani ya chupa.
usije ukasahau ukatia sukari! Chungu ndio tamu.kahawa chungu(thungu) aiwekwi sukari
Waeza kunywa na vishete, mlenge au mitahi, vile utakavyopenda.
'Waraibu' wa kinywaji hiki husema njugu hufanya 'maajabu' unapoambatisha na kahawa thungu.
0
0
0