logo

Ziidi vs. other MMFs vs. Savings: Where Should Your Hustle Money Go?

Screenshot of Zidii dashboard

By Paul Githinji

Kenya’s youth are on a grind – from side gigs to hustles – and every shilling counts. Enter Money Market Funds (MMFs), an innovative way to grow your cash. One new player is Safaricom Ziidi, which lets you park as little as KES 100 straight from M-PESA and promises daily interest. But how does it stack up against other Kenyan MMFs, and also against SACCOs or bank savings accounts?

Do you want the complete guide to Money Market Funds in Kenya? Check it out here.

Disclaimer: All investments carry risk. Never invest money you can’t afford to lose. MESH doesn’t earn a shilling from Safaricom or any other MMF—we’re here to keep it 💯 with you!

Opportunity banner image
Opportunity banner image

FYI 🧠: Hapa Kenya 🇰🇪, sio every Money Market Fund (MMF) 💰 hu-update interest rates daily 📉📈. For example, some like Ziidi MMF update rates zao kila siku 🗓️, so utaona returns zako zikichange live-live kupitia the M-PESA App and USSD⚡. But MMFs zingine hawafanyi hivyo – nyingi hu-update rates once a week 🕒 au monthly 📆. So, don’t worry😅 ukiona hakuna published daily changes kwa other funds.

Table Breakdown: What Should Meshers Know? 👆📊💰🔥🚨

1. Accessibility & Thresholds: Who Lets You Start Small?

Ziidi

● You can start with 100 bob tu. Ni boda fare level—haina “minimum balance” drama.

● Ni easy kuingia. Weka doh kwa M-Pesa then upige (*334#), au utumie M-Pesa app. Click, confirm, invest—Ni easy kama kutuma text.

Other MMFs (CIC, Sanlam, Britam, Kuza)

● Most zinataka minimum balance ya 1,000–5,000 bob. Unfortunately, watu wengi hawawezi start kama hawana surplus funds kama hizo.

● MMF zingine zitataka ujaze forms, utoe copy ya ID, na labda office visits. Ni time killer for hustlers who need every minute kupiga biz.

SACCOs

● SACCOs often ask kila member atoe an entry fee of 500–1,000 bob. Then you and family ama close group can save and borrow pamoja kama members wa the same SACCO.

● Ukipata hio entry fee, just sign the register, flash ID yako, then ufuata group rules kama pro.

Banks (Savings & Fixed Deposits)

● Savings: KES 1,000+ kwa account ya kawaida.

● Fixed deposit: KES 10,000+ kamwe.

2. Ease of Use: M-Pesa vs. Old-School Hassle

Ziidi

● Unatumia phone yako kufanya kila kitu—hakuna office queues au paperwork ya kusumbua.

● Withdrawals ni instant via M-Pesa. Kama kuna emergency, utatoa pesa yako chap-chap.

Other MMFs

● CIC MMF: Unaweza pull out funds bila penalty, but kuna 1–2 days processing before upate funds.

● Sanlam MMF: Withdrawal inaweza take hadi three business days ku-reflect. Kuna one free withdrawal kila mwezi; after that ni 500–750 per extra withdrawal.

● Britam MMF: Hakuna penalties ukitoa pesa yako. Pia, funds zinaingia M-Pesa au bank account yako within 48 hours.

● Kuza MMF: Ina-allow unlimited withdrawals, but funds zinakuja within two working days.

● Some MMFs charge “early-exit” fines kama unatoa before maturity—ni wise kucheki terms zao before signing.

SACCOs

● Lazima utoe notice ya 7–14 days kabla ya kutoa your savings.

● Itabidi upige njia to their offices kufanya withdrawals, coz you’ll need kujaza forms au ku-sign register book.

Banks

● Savings accounts: Withdrawals ni instan via ATM au app—hakuna drama mob.

● Fixed deposits: Ziko locked hadi maturity. Uki-choose kutoa mapema, interest yote una-forfeit; partial withdrawals sio allowed bila ku-break deposit.

What Does This Mean?

➣ If unataka convenience ya instant withdrawal at any time, chagua Ziidi.

➣ If uko fine waiting 1–3 days, chagua one of the other Money Market Funds, but jaribu ku-find ile itakupea interest poa.

➣ If you can plan weeks ahead, ku-join SACCO ni bet poa.

➣ If unataka instant access or a long-term lock, pick bank savings ama fixed deposits.

3. Fees & Hidden Costs: Who’s Eating Your Profit?

Ziidi

Unataka kucheza na Ziidi? If so, utaona:

● Kuna 2 % management fee itakatwa from interest yako kila mwaka.

● Hakuna charges za withdrawal—deposit na withdraw zote ni free via M-Pesa.

● Ile interest utapata iko subject to 15 % tax ya KRA.

Other MMFs (CIC, Sanlam, Britam, Kuza)

● Most wana-charge 1.5 %–2.5 % annual management fee on interest ile umevuna.

● Some, like Sanlam MMF, zina-charge switching fees au transaction charges uki-move investment yako from one fund to another.

● Britam, for example, inaweza chukua up to 2.5 % on returns, so check kila MMF’s brochure carefully.

SACCOs

● Kila SACCO iko na membership fee—for example, Ushuru Sacco ina-charge 1K entrance fee.

● Kuna withdrawal fee ndogo ukitoa pesa before the expiry of the notice period.

● Kama unataka loan, utatoa processing fee ya 1 %–2 % of the loan amount (depending on the SACCO you join).

Banks (Savings & Fixed Deposits)

● Savings accounts: Usually hakuna management fee; ATM/app withdrawals ni free au cheap sana.

● Fixed deposits: Funds zako ziko locked till maturity. Ukitoa mapema, utapoteza interest yote.

4. Flexibility & Lock-In: Lock Funds or Stay Liquid?

Ziidi

● Uko na option ya ku-lock funds for 72 hrs—hii ni ideal for impulse control coz utapata time yak u-reflect kama you really need to withdraw immediately.

● Baada ya buffer ya 3 days, you can unlock anytime bila fine.

Other MMFs

● CIC MMF: Withdrawals clear in 1–2 days, bila penalties, na pia you can switch or transfer anytime.

● Sanlam MMF: Funds zita-drop kwa account yako in up to 3 business days. Utapata one free withdrawal kila month, then watakula 500–750 bob for extra withdrawals. Ni poa coz itafanya uwache ku-withdraw all the time.

● Britam MMF: Kuna initial 14 -day lock, then withdrawals ni within 48 hrs

● Kuza MMF: They allow unlimited withdrawals, lakini kuna 3-month lock-in on some share classes; funds zako zita-clear in 1–2 days afterward.

SACCOs

● Kila SACCO iko na a specific notice period (usually 1–3 months) before uweze ku-withdraw your full balance.

● Withdrawal pia zinahitaji office visit, kujaza form, na ku-sign register.

Banks

● Savings: Ziko liquid, so unaweza toa pesa anytime via ATM/app—kuingia banking hall na kupiga line sio lazima.

● Fixed deposit: Hizi accounts ziko na strict lock-in hadi the chosen term; early exit forfeits interest (no partial withdrawals).

Cheza fiti na ile investment option inaingiana na vibe au hustle yako—instant access, short waits, or long-term lock-in. Hustle smart!

5. Risk & Returns: Who’s Chilling, Who’s Sweating?

Ziidi & Other MMFs

Money market funds ni low-risk compared to stocks. Wanaweka pesa yako kwa T-bills na commercial paper—hizi ni short-term government na corporate debts ambazo hazibounce sana. Daily yields za MMFs range ..., so ni poa uchague the best one for you.

For example, Madison Group ina-offer interest rates zina-range from 12%-15 %, yet Equity Money Market Fund ilipea investors interest ya about 6% on 7th May 2025. Lakini, ni poa kukumbuka zinawezabounce kulingana na treasury rates na performance ya financial market.

SACCOs

SACCOs ziko na medium risk—kama members wengine hawalipi loans zao, dividends zinaweza enda down kiasi. Lakini bado, members wanapata dividends of 10%–2...., pamoja na interest kidogo kwa savings zao.

Banks

Savings accounts ni super safe— Unajua ile story ya bank kufail? Usijali, KDIC (Kenya Deposit Insurance Corporation) iko na wewe. Wana-protect deposits zako ... kwa kila bank account. This means bank yako ikicrash utalipwa hadi hiyo amount.

Hii ina-cover all types of deposit accounts—current, savings, fixed deposits, na hata foreign currency accounts. So, whether uko na account ya kulipwa salary ama ya kuweka savings zako, uko covered kama doh yako ziko below 500k.

Fixed deposits zinatoa guaranteed returns of about 7%–11% p.a., na hazina volatility mob—lakini hutaweza kuaccess pesa hadi maturity ama ulipie penalty ukitoa mapema.

6. What Fits Your Hustle?

Ziidi:

Unataka investing ya haraka na ndogo? Anza na KES 100, swipe kwa simu yako, and withdraw instantly via M-Pesa. Hii MMF ni poa for emergencies au kujaribu maji.

Other MMFs (CIC, Sanlam, Britam, Kuza)

Uko na KES 1,000–5,000 ya kucheza nayo? Hizi funds zinakuruhusu kufuata higher ceilings kama uko na patience ya 1–3 day withdrawals na huna shida na short lock-in kwa zingine.

SACCOs

Unataka nguvu ya group na access ya affordable loans? Jiunge na SACCO, save na watu wako, na upate juicy dividends—lakini kuwa ready ku-wait weeks for withdrawals.

Banks

Unataka tu kuweka pesa safe as you earn some interest? Savings accounts zinakupa instant access via ATM au app bila drama. Fixed deposits zinakufungia pesa hadi maturity for better rates kama unaweza chill a few months or even years.

ro Tip: Chagua kulingana na vile pesa yako iko, convenience, na risk unaweza handle. Hustle smart, invest smart! 😎💸

Meshers, Let’s Stack Paper! 💡💰

MESH fam, sasa you know the difference between MMFs, SACCOs, na bank savings accounts. Tusaidiane kujua the best mix ya kucheza na doh depending na goal ya kila mtu.

If bado uko guest mode, joining MESH ni one of the smartest moves unaweza make as a young hustler, coz:

● Utapata more real-life stories from fellow MESHERS.

● You will meet other hustlers wale mnaweza jengana.

● Utaget free tips na guides za kupiga steps za nguvu.

● Utaingia community ya hustle-minded youth kama wewe with amazing hustle strategies and daily discussions.

Cheki, Meshers wanapenda ku-explore hustle na kujengana! Tunapenda ku-push pesa & connections. Join squad, tufungue njia pamoja! 💪🏾 For example, the recent MESH BIZ Live classes 1 to 6 zilikuwa fire na tulichanuka sana mambo ya biz! 🔥

Sign up free – future yako itakushukuru.

#TujenganeMESH #HustleSmart #SideHustleSavings #MtaaniInvesting #MeshInvestmentHustle #MESHTips #GoodInvestmentKenya #MoneyMarketFunds #DigitalHustler254 #FinancialGrowth254

Need a business loan?💰

Types of Business Loans in Kenya